Rais Dkt. Mwinyi avutiwa na soko la dagaa Geita

0
175

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduizi, Dkt. Hussein Mwinyi amesema kuwa serikali ya umoja wa kitaifa iliyoundwa visiwani Zanzibar inalenga kukuza umoja na ushirikiano baina ya wananchi wa visiwa hivyo.

Dkt. Mwinyi amesema hayo mapema leo alipotembelea soko la Dagaa mkoani Geita baada ya kufanya mazungumzo na Rais wa Tanzania, Dkt. John Magufuli.

Katika hatua nyingine amesema kuwa soko hilo la dagaa alilolitembelea limekuwa funzo kwamba wanaweza kuwa na soko kama hilo Zanzibar.

Pia amesisitiza kuendelezwa kwa ushirikiano baina ya wananchi wa pande zote za muungano akisema kuwa Zanzibar kuna Wasukuma wengine na hivo hivyo mkoani Geita kuwa wakazi wengi kutoka Pemba na Unguja.