Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amemteua Hemed Suleiman Abdulla kuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee imeeleza kwamba Rais Dkt. Hussein Mwinyi amemteua Hemed Suleiman Abdulla kuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwa mujibu wa uwezo aliyopewa chini ya Kifungu Namba 39 (1) na 39 (2) cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.
Kabla ya Uteuzi huo Hemed Suleiman Abdulla alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba.
Uteuzi huo umeanza leo tarehe 08 Novemba, 2020.