Rais Dkt. Mwinyi arejea nchini kutoka Maputo

0
171

Rais wa Zanzibar  na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi, amerejea nchini akitokea nchini Msumbiji alikokwenda kumwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan kwenye mkutano wa Wakuu wa nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

Katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume huko Zanzibar, Rais Dkt. Mwinyi na ujumbe wake amepokelewa na viongozi mbalimbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na wale wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mkutano huo wa SADC uliofanyika mjini Maputo, pamoja na mambo mengine umejadili mikakati ya kukabiliana na vikundi vyenye silaha ambavyo katika siku za hivi karibuni vimekuwa vikifanya mauaji ya kikatili dhidi ya raia katika maeneo mbalimbali nchini Msumbiji.

Mapema katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Malavane Maputo nchini Msumbiji,Rais Mwinyi akiwa  na mkewe Mama MARIAM MWINYI na Ujumbe aliofuatana nao waliagwa kwa Gwaride rasmi la jeshi la nchini humo.