Rais awataka viongozi kuendelea kuwahimiza waumini kujikinga na magonjwa

0
197

Rais Samia Suluhu Hassan amewataka viongozi wa dini kuendelea kuwakumbusha waumini kujikinga na magonjwa ya milipuko ikiwemo Ebola ambao umeingia nchi jirani na Tanzania.

Rais Samia amesema hayo katika Baraza la Maulid linalofanyika kitaifa katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam ambapo amesema viongozi hao wasichoke kuwakumbusha waumini juu ya kujikinga na magonjwa.

“Tunashukuru viongozi wa dini wapo bega kwa bega na Serikali katika kuwakumbusha wananchi juu ya masuala mbalimbali, kwenye sensa mlikuwa nasi, kwenye uviko pia, naamini Wizara ya Afya itaendelea kushirikiana nanyi ili kuwakumbusha kujikinga na Ebola,” amesema Rais Samia.

Katika hatua nyingine amewakumbusha wazazi juu ya kuwalea watoto katika maadili ikiwemo kuwapeleka madrasa ili wajifunze maadili ya Uislamu.