Rais awaapisha Viongozi Ikulu

0
144

Rais Samia Suluhu Hassan leo amewaapisha Viongozi mbalimbali aliowateua hivi karibuni katika hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma.

Miongoni mwa Viongozi hao ni Mawaziri watatu kufuatia mabadiliko madogo katika Baraza la Mawaziri aliyoyafanya.

Mawaziri walioapishwa ni
George Simbachawene kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Bunge, Sera na Uratibu na Damas Ndumbaro aliyeapishwa kuwa Waziri wa Katiba na Sheria.
 
Mwingine aliyapishwa ni Pindi Chana kuwa Waziri Maliasili na Utalii.

Mara baada ya Viongozi hao kuapishwa na Rais Samia Suluhu Hassan, walikuwa kiapo cha Uadifu kwa Viongozi.

Hafla hiyo imehudhuriwa pia na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson.