Rais awaapisha Mawaziri, Naibu Mawaziri

0
153

Rais Samia Suluhu Hassan, leo amewaapisha Mawaziri na Naibu Mawaziri aliowateua hivi karibuni.

Hafla ya kuwaapisha Mawaziri na Naibu Mawaziri hao imefanyika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali.

Miongoni mwa Viongozi waliohudhuria hafla hiyo ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahimu Juma, Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson na baadhi ya viongozi wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama

Mawaziri walioapishwa ni pamoja na Nape Nnauye anayekuwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Hamad Masauni anayekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt, Pindi Chana ameapishwa kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, Hussein Bashe anakuwa Waziri wa Kilimo na Dkt. Angelina Mabula ameapishwa kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Wengine walioapishwa hii leo na Rais Samia Suluhu Hassan ni Antony Mavunde kuwa Naibu Waziri wa Kilimo, Jumanne Sagini kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt. Lemomo Ole Kiruswa ameapishwa kuwa Naibu Waziri wa Madini, Atupele Mwakibete kuwa Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi anayeshughulikia sekta ya Uchukuzi na Ridhiwan Kikwete ameapishwa kuwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.