Rais awaapisha aliowateua

0
140

Rais Samia Suluhu Hassan, leo amewaapisha Mawaziri wanne pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kufuatia uteuzi alioufanya hapo jana.

Mawaziri walioapishwa katika hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma ni Dkt. Stergomena Tax kuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa,  Dkt. Ashatu Kijaji kuwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na  January Makamba kuwa Waziri wa Nishati.

Wengine walioapishwa ni Profesa Makame Mbarawa kuwa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi na Dkt. Eliezer Feleshi ambaye ameapishwa kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

 Hafla ya kuapishwa kwa Mawaziri hao pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali imehudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai.