Rais atoa pole kifo cha Rupia

0
222

Rais Samia Suluhu Hassan ametoa salam za pole kufuatia kifo cha Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu Balozi Paul Rupia ambaye amefariki dunia leo akiwa na umri wa miaka 84.

Kwenye salamu zake Rais Samia amesema katika uhai wake, Balozi Rupia alitoa mchango mkubwa katika masuala ya kidiplomasia, mageuzi ya kiuchumi na utumishi wa umma.