Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Dkt. Boniphace Luhende kuwa Wakili Mkuu wa Serikali.
Kabla ya uteuzi huo Dkt. Luhende alikuwa Naibu Wakili Mkuu wa Serikali.
Dkt. Luhende anachukua nafasi ya Gabriel Malata ambaye aliteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu.
Pia Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Sarah Mwaipopo kuwa Naibu Wakili Mkuu wa Serikali.
Kabla ya uteuzi huo Mwaipopo alikuwa Wakili wa Serikali Mkuu katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Mwaipopo anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Luhende ambaye ameteuliwa kuwa Wakili Mkuu wa Serikali.
Uteuzi huo umeanza Oktoba 9 mwaka huu.