Rais atengua uteuzi Mkurugenzi Mkuu TPDC

0
193

Rais Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Thobias Mwesiga ambaye aliteuliwa jana Aprili 4, 2021.

Kufuatia uamuzi huo Rais Samia amemrejesha Dkt. James Mataragio kuwa Mkurugenzi Mkuu wa TPDC.

Dkt. Mataragio ndiye aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa TPDC kabla ya uteuzi wa Mwesiga.

Taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu imeeleza kuwa Dkt. Mataragio anaendelea na majukumu yake mara moja.