Rais amlilia Mkurugenzi Igunga

0
176

Rais Samia Suluhu Hassan ameeleza kusikitishwa na kifo cha Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Igunga mkoani Tabora, Fatuma Omar Latu pamoja na dereva wake aliyetambuliwa kwa jina la Alex.

Vifo hivyo vimetokewa hapo jana mkoani Mbeya walipokuwa safarini wakitokea mkoani humo, ambapo Mkurugenzi huyo alikuwa akishiriki katika mkutano wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa (ALAT).

Katika ukurasa wake wa twitter, Rais Samia Suluhu Hassan ameandika “Mungu azilaze roho zao mahali pema peponi. Amin.”