Rais Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa Viongozi mbalimbali ambapo amemteua Sophia Simba kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Magavana wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii (ISW)
Sophia Simba ni Mbunge Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Jaji Hamisa Hamisi Kalombola ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma, huku Obey Assery akiteuliwa kuwa Mwenyikiti wa Bodi ya Usimamizi wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC).
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais – Ikulu,
uteuzi huo unaanza mara moja.