Rais Samia Suluhu Hassan ameiagiza wizara ya Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki kuangalia namna ya kuendeleza maeneo yanayomilikiwa na Tanzania Katika mataifa mbalimbali badala kuyaacha yakikaa bila kutumika kwa muda mrefu.
Rais Samia Suluhu Hassan ametoa agizo hilo mkoani Dar es Salaam mara baada ya kuzindua jengo jipya la makao makuu ya benki ya CRDB.
Amesema maeneo hayo yanaweza kutumika katika uwekezaji wa miradi mbalimbali na kuliingizia Taifa fedha za kigeni.
Rais Samia Suluhu Hassan amesema moja ya faida ya safari yake Falme za Kiarabu ni Tanzania kusaini mkataba wa biashara ya mbogamboga kutoka Tanzania kwenda Dubai.
“Niwapongeze sana CRDB Bank mmekuwa walipa kodi wazuri na mmekuwa mkifanya vizuri sana katika kutoa huduma za kibenki kwa Watanzania, nawapongeza kwa kulipa kodi ya bilioni 249.2, hii inaonesha mnapata faida.” amesema Rais Samia Suluhu Hassan
Aidha ameipongeza benki ya CRDB kwa kurasimisha sekta binafsi hasa wafanyabiashara wadogo ili wajiendeshe kitaalam na waweze kukopeshana.
Rais Samia amesema Serikali itaendelea kutafuta Wawekezaji wa ndani na nje ili wawekeze kwenye miradi mbalimbali yenye manufaa kwa Watanzania