Askari wanaomuunga mkono mbabe wa kivita nchini Libya, -Khalifa Haftar wamewateka nyara watu wawili raia wa Uturuki, na kusababisha taharuki ya Kimataifa.
Sababu za askari hao kuwashikilia mateka raia hao wa Uturuki haifahamiki, lakini Jumatatu wiki hii Rais Reccep Tayyip Ordegan wa nchi hiyo alisema kuwa hatua ya Khalifa kuendelea na mashambulio mjini Tripoli ni jaribio la Mapinduzi.
Ordegan alisema kuwa kitendo cha mbabe huyo wa kivita nchini Libya kuwashambulia raia na kujaribu kuutwaa mji wa Tripoli ni jaribio la Mapinduzi dhidi ya serikali halali ya nchi ya Libya.
Khalifa amekuwa akiomba msaada wa Kimataifa kuendelea na mapambano yake mjini Tripoli dhidi ya serikali ya mpito ya nchi hiyo.
Hadi sasa watu 340 wamekufa nchini Libya, ikiwa ni takribani mwezi mmoja sasa tangu Haftar na askari wake walipokwenda mjini Tripoli kujaribu kutwaa madaraka.