Raia wa China waadhimisha Siku ya Taifa hilo

0
100

Rais John Magufuli amempongeza Rais Xi Jinping wa China na Raia wote wa nchi hiyo, kwa kuadhimisha miaka Sabini ya Taifa hilo.

Katika salamu hizo za pongezi alizotuma kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter, Rais Magufuli amesema kuwa, Tanzania itaendelea kudumisha ushirikiano na urafiki uliodumu kwa muda mrefu baina ya Mataifa hayo mawili.

Rais Magufuli ametumia pia lugha ya Kichina katika kutoa pongezi hizo yanayosomeka kama
祝贺习近平主席!祝贺全体中国人民, yakiwa na maana kuwa “Hongera Kiongozi, hongera Wachina wote”.