Rais ataka alama daraja la Tanzanite lisadifu jina lake

0
302

Rais Samia Suluhu Hassan ameagiza kubadilishwa kwa alama ya Mwenge wa Uhuru iliyowekwa juu ya daraja la Tanzanite na kuwekwa kwa alama itakayoendana na jina lililopo sasa.

Rais Samia ametoa agizo hilo mkoani Daf es Salaam wakati akifungua rasmi daraja la Tanzanite ambalo lilianza kutumika Februari Mosi mwaka huu.

“Ushauri niliopata kwa Wananchi daraja hili tunaliita daraja la Tanzanite lakini alama tuliyoiweka ni alama ya mwenge. Pamoja na kutambua kwamba mwenge ni tunu yetu adhimu, Wananchi wangependa sana kuona umbo la Tanzanite pale ulipo mwenge ili kukamilisha jina la daraja hili,” amesema Rais Samia Suluhu Hassan

Daraja jipya la Selander (Tanzanite) lina urefu wa kilometa 1.03 na barabara unganishi zenye urefu wa kilometa 5.2.