Radi yasababisha vifo Geita

0
1900

Wanafunzi sita wa shule ya msingi Imako wilayani Geita wamekufa baada ya radi kupiga katika shule hiyo mapema leo Jumatano Oktoba 17.

Kaimu Mkuu wa mkoa wa Geita, Josephat Maganga amewaambia waandishi wa habari mkoani Geita kuwa wanafunzi 21 na walimu wawili wa shule hiyo ya Imako wamejeruhiwa katika tukio hilo.

Amesema majeruhi wanapatiwa matibabu kwenye Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Geita.