RAAWU watakiwa kuwa mfano wa kuigwa

0
123

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson, amekitaka Chama cha Wafanyakazi (RAAWU) kuwa mfano kwa vyama vingine kwa kuwa ndani yake kuna watafiti na wanahabari ambao wana mchango mkubwa katika ujenzi wa Taifa.

Akizungumza mkoani Mbeya katika ufunguzi wa semina kwa viongozi wa matawi ya RAAWU , Dkt Tulia ameahidi kuzibeba changamoto za Wafanyakazi hao na kuzifikisha sehemu husika ili zipatiwe ufumbuzi.

Kwa upande wake Katibu mkuu wa RAAWU Taifa Winston Makere ameiomba Serikali kuunda chombo kimoja kitakachoshughulikia migogoro ya Wafanyakazi, na kujenga umoja na ushirikiano baina ya utawala na Viongozi wa vyama kwenye sehemu zao za kazi.

Baadhi ya viongozi wa matawi ya RAAWU wamezungumzia changamoto za Wafanyakazi na kuwataka viongozi wa chama hicho Taifa kuendesha mafunzo kwa Wanachama waliopo kwenye matawi nchini, ili kudumisha umoja kwa Wafanyakazi.