Pwani yatakiwa kuboresha miundombinu ili kuvutia Uwekezaji wa Viwanda

0
309

Waziri MKuu Kassim Majaliwa amewaagiza viongozi wa mkoa wa Pwani pamoja na wa wilaya zote mkoani humo, kuhakikisha wanapeleka miundombinu muhimu kwenye maeneo vinapojengwa Viwanda.

Akifungua maonesho ya Viwanda na Biashara mkoani Pwani yanayofanyika pamoja na Kongamano la Uwekezaji la mkoa huo, Waziri Mkuu Majaliwa amesema kuwa, miundombinu hiyo ambayo ni pamoja na maji na umeme ni muhimu kwa uanzishwaji na ukuaji wa viwanda hivyo.

Ameongeza kuwa, hatapenda kusikilia kuna Mwekezaji yeyote anayetaka kujenga viwanda katika mkoa wa Pwani anashindwa kufanya hivyo kutokana na kukosekana kwa miundombinu ya uhakika.