Mhadhiri Mstaafu wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam Prof. Issa shivji amemuelezea Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, kama kiongozi aliyependa haki na kuamini katika Usawa wa watu na haki zao.
Prof. Shivji ametoa maelezo hayo wakati akitoa mada kuhusu maisha ya Mwalimu Nyerere katika Mdahalo wa Kitaifa wa kuadhimisha miaka 100 ya Kuzaliwa kwa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere unaofanyika katika Shule ya uongozi ya Mwalimu Nyerere iliyopo Kibaha, Mkoani Pwani.
Shivji amsema, Mwalimu alikuwa haamini kuwa tajiri na masikini wako sawa katika sekta ya haki ama sheria hivyo alianzisha falsafa ambazo zililenga katika kuwapa haki watu bila kuwabagua.
Ameongeza kuwa akiwa madarakani Mwalimu alianzisha falsafa ya siasa ya Ujamaa na Kujitegemea ambayo ililenga kutoa nafasi kwa kila Mtanzania kushiriki katika kuzalisha mali.