Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa amechukua fomu ya kuwania Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Profesa Mbarawa amechukua fomu leo asubuhi katika Ofisi Kuu ya CCM Zanzibar Kisiwandui, ambako alikabidhiwa fomu hiyo na Katibu wa Oganaizesheni wa Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Galous Nyimbo.
Profesa Mbarawa anakuwa mwanachama wa 10 wa CCM kuchukua fomu ya kuwania kiti cha Urais wa Zanzibar tangu zoezi hilo lilipoanza Jumatatu wiki hii.