Profesa Kitila Mkumbo afanya ziara kwenye maonesho ya Expo 2020 Dubai

0
131

Waziri wa Viwanda na Biashara, Profesa Kitila Mkumbo leo Desemba 17,2021 ametembelea banda la Tanzania, Oman na Thailand kwenye Maonesho ya Dunia ya Expo 2020 Dubai yanayoendelea mjini Dubai.

Katika ziara hiyo, waziri Mkumbo ameongozana na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja , Balozi wa Tanzania katika Umoja wa Falme za Kiarabu, Mohamed Mtonga na Mkurugenzi wa Diplomasia ya Uchumi, Balozi Edwin Rutageruka.

Akiwa katika banda la Tanzania Profesa Mkumbo amezungumza na washiriki kutoka nchini Tanzania na kuwataka kuangalia namna ya kuboresha banda hilo pamoja na kuweka mikakati ya kuvutia wawekezaji nchini Tanzania.

Aidha, Profesa Mkumbo amewataka washiriki hao kujiandaa vyema kwa ajili ya “ Tanzania Day ” itakayofanyika 26 Februari 2022 ambayo inalenga kuitangaza Tanzania katika uwekezaji, utalii na biashara.

Katika mabanda ya Oman na Thailand waziri Mkombo amejionea namna ambavyo teknolojia imetumika katika kuonesha mafanikio na uwekezaji uliopo katika nchi hizo.