Prof. Mbarawa: Mlango wa ndege ulifunguliwa na mhudumu

0
134

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa ametoa ripoti ya awali ya uchunguzi wa ajali ya ndege ya Precision Air iliyotokea tarehe 6 mwezi huu Bukoba mkoani Kagera na kusababisha vifo vya watu 19.

Ripoti hiyo imeonesha kuwa mlango wa ndege hiyo ulifunguliwa na mhudumu wa ndege kwa msaada wa abiria.

Profesa Mbarawa amewaambia waandishi wa habari mkoani Dar es Salaam kuwa, wananchi waliokuwa wanafanya shughuli za uvuvi jirani na eneo la ajali walifika eneo la ajali dakika 5 baada ya ndege hiyo kuanguka.

Amesema wananchi hao waliendelea na juhudi za kufungua mlango kwa nje, hali iliyompa ujasiri mhudumu wa ndege hiyo ya Precision Air na abiria kufungua mlango huo baada ya kuona nje kuna msaada ambao unaweza kuwasaidia.