Posho, madaraja, mishahara kupanda

0
218

Rais Samia Suluhu Hassan amesema zoezi la kuboresha maisha ya wafanyakazi nchini katika sekta mbalimbali ni endelevu.

Rais Samia ametoa kauli hiyo mkoani Morogoro wakati akihutubia katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani.

Amesema mbali na kuongezwa kwa asilimia 23 ya mishahara ya kima cha chini mwaka 2022, kwa mwaka 2023 na kuendelea Wafanyakazi nchini wataendelea kupandishwa vyeo, madaraja, viwango vya posho pamoja na mishahara.

“Tumejiandaa pia kupandisha madaraja…vyeo vitaendelea kupandishwa, ‘recategorization’ itaendelea kufanywa, yale madaraja ya mserereko ambao hawakupata mwaka uliopita mserereko upo mwaka huu. Lakini niseme pia kuna nyongeza za mishahara za mwaka ambazo kwa muda mrefu zilikuwa zimesitishwa, nikaona mwaka huu tuzirudishe.” Amesema Rais Samia na kuongeza kuwa
“Wafanyakazi wote mwaka huu mbali na niliyoyasema… kuna nyongeza za mishahara za kila mwaka. Tunaanza mwaka huu na tutakwenda kila mwaka kama ilivyokuwa hapo awali.”