Polisi wawaua kwa risasi majambazi watatu

0
264

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam limefanikiwa kuwaua majambazi wa watatu na kukamata silaha moja aina ya bastola iliyofutwa namba pamoja na magazine iliyokuwa na risasi moja.

Tukio la kuuawa kwa majambazi hao lilitokea jana Januari 19 eneo la Magomeni baada ya askari waliokuwa doria kuwapiga kwa risasi majambazi hao katika majibizano ya silaha, na walifariki dunia wakati wakiwahishwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa ajili ya matibabu.

Kwa mujibu wa taarifa ya polisi, uchunguzi wa awali umebaini kuwa majambazi hao wamekuwa wakifanya matukio mbalimbali ya kihalifu maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salama na mikoa ya jirani.

Jeshi la polisi linaendelea na msako mkali wa wahalifu wote wanaofanya uhalifu katika maeneo mbalimbali, na limewasihi wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu.