Polisi wasisitiza amani siku ya Eid

0
137

Jeshi la polisi nchini limewahakikishia Waumini wa dini ya Kiislam na Watanzania wote hali ya ulinzi na usalama katika kusherehekea sikukuu ya Eid Al Adha hapo kesho.

Katika taarifa yake, Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini David Misime amesema jeshi hilo litawachukukulia hatua kali wake wote wakataojaribu kuvuruga hali ya amani wakati wa sikukuu hiyo.

Amewataka wale wote wenye tabia ya kuwashawishi wengine kufanya vitendo vya uhalifu kuacha tabia hiyo mara moja, kwani nao pia watachukuliwa hatua.