Polisi waagizwa kusambaratisha madanguro

0
228

Mkuu wa mkoa wa Mtwara Kanali Ahmed Abbas ameliagiza Jeshi la Polisi mkoani humo kusambaratisha mara moja madanguro, ambayo yameanza kushika kasi mkoani humo.

Kanali Abbas
ametoa agizo hilo wakati wa kikao cha Kamati ya Ushauri ya mkoa baada ya wajumbe kutoa hoja ya kuwepo kwa madanguro katika baadhi ya maeneo ya manispaa ya Mtwara, Mikindani ambayo kwa kiasi kikubwa ni chanzo cha watoto kuacha shule.

Aidha Kanali Abbas amesema haiwezekani kuona hali hiyo inaendelea katika mkoa wa Mtwara na kutaka wahusika wote wachukuliwe hatua.