Kamanda wa polisi wa mkoa wa Arusha, Justine Masejo amesema jeshi hilo kupitia kikosi cha mbwa na farasi, limejipanga kukabiliana na dawa za kulevya pamoja na vilipuzi vya aina yeyote mkoani humo.
Kamanda Masejo ametoa kauli hiyo mkoani Arusha alipotembelea kikosi hicho, lengo likiwa ni kukagua mazoezi ya mbwa wanaotumiwa na jeshi la polisi kuwatambua wahalifu wakiwemo wa dawa za kulevya, silaha pamoja na mabomu.
Amesema jeshi la polisi mkoani Arusha kupitia kikosi cha mbwa na farasi kinatoa mafunzo kwa mbwa wa kiraia, ili kuimarisha ulinzi na usalama katika mkoa huo.
Kwa upande wake mkuu wa kikosi cha mbwa na farasi mkoa wa Arusha, William Mwaisumo amesema, kikosi hicho kimejipanga vema kutoa mafunzo kwa mbwa wote watakaopelekwa kikosini hapo kwa ajili kupatiwa mafunzo ya ulinzi.