Polisi kukagua shule zote kudhibiti moto

0
279

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene ameliagiza Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kufanya ukaguzi katika shule zote nchini, ili kubaini iwapo kuna vihatarishi vinavyoweza kuwa vyanzo vya moto.

Simbachawene ametoa agizo hilo mkoani Arusha wakati akitembelea baadhi ya maeneo ya taasisi zilizo chini ya wizara anayoiongoza, ikiwa ni hatua za kudhibiti matukio ya shule kuungua moto ambayo yamekuwa yakihatarisha maisha ya wanafunzi na kuharibu mali zao na za shule.

Pia amelisisitiza jeshi hilo kufanya ukaguzi wa mara kwa mara katika visima vya maji ya Zimamoto, na kuhakikisha wapo tayari kukabiliana na ajali za moto muda wowote zinapotokea.