POLISI KUIMARISHA USALAMA UCHAGUZI WA 2024, 2025

0
149

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Camillus Wambura amesema, Jeshi hilo limekwishaanza maandalizi ya kuimarisha ulinzi na kusimamia usalama katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka 2024 na uchaguzi Mkuu mwaka 2025.

IGP Wambura ameyasema hayo mkoani Dar es Salaam, alipokuwa akizungumza katika ufunguzi wa mkutano mkuu wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi Nchini.

Amesema katika mkutano unaozinduliwa hii leo wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi, moja ya mikakati na mipango itakayojadiliwa ni pamoja na hilo la ulinzi na usalama wakati wa chaguzi hizo.

Aidha, IGP Wambura amesema Jeshi la Polisi nchini linaendelea kuhakikisha kunakuwa na usalama katika miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali ili kudhibiti wizi wa vifaa pamoja na hujuma.