Polepole, Gwajima Jerry Silaa kuhojiwa

0
163

Kamati kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa iliyoketi chini ya mwenyekiti wa chama hicho Samia Suluhu Hassan imepokea na kujadili taarifa za mwenendo wa Wanachama na Viongozi wake watatu (3) wa CCM ambao na kukubaliana kuwaita ili wapate nafasi ya kusikilizwa.

Wanachama walijadiliwa na kutakiwa kujieleza ni pamoja na mbunge wa Ukonga, Jerry Silaa, Mbunge wa Kawe Josephat Gwajima na Mbunge wa kuteuliwa Humphrey Polepole

Taarifa iliyotolewa na Katibu wa (NEC) itikadi na uenezi wa CCM Shaka Hamdu Shaka imeeleza kuwa baada ya Kuzingatia kwa kina taarifa hiyo, Kamati Kuu imeazimia kuwaita Viongozi hao, ili kuwapa fursa ya kuwasikiliza kama inavyoagizwa na Kanuni za Uongozi na Maadili, Toleo la Mwaka 2017 na Katiba ya CCM ya Mwaka 1977, Toleo la 2020 .