PM aomboleza kifo cha Mwl. Kashasha

0
133

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametuma salamu za pole kwa familia na wapenzi wa soka nchini kufuatia kifo cha mchambuzi nguli wa soka nchini Mwalimu Alex Kashasha.

Ameeleza kuwa Mwalimu Kashasha ameacha pengo kubwa kwenye michezo kama mwalimu bora wa michezo, na kuwaomba wanafamilia na wapenzi wa michezo kuendelea kumuombea.

Aidha, Waziri Mkuu amesema Mwalimu Kashasha atakumbukwa kwa ustadi wake wa kuchambua mechi za soka mbashara, pamoja na vipindi vya maelezo ya mechi za soka za ndani na nje ya nchi.

Mwalimu Kashasha aliyekuwa mtumishi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), alifariki dunia tarehe 19 mwezi huu katika hospitali ya Kairuki mkoani Dar es Salaam na kuzikwa jana katika makaburi ya KinoƱdoni mkoani Dar es Salaam.