Pingamizi la Mbowe na wenzake latupiliwa mbali

0
104
Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe akizungumza na wandishi wa habari, bungeni mjini Dodoma jana. Picha na Emmanuel Herman

Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi imetupilia mbali pingamizi lililowasilishwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe na wenzake la kutaka kesi inayowakabili isisikilizwe na mahakama hiyo kwa kuwa haina mamlaka ya kusikiliza kesi zenye mashtaka ya ugaidi.

Uamuzi huo umetolewa leo na Jaji Elinaza Luvanda ambaye baada ya kupitia hoja za pande zote mbili amesema Mahakama yake ina mamlaka ya kusikiliza mashauri ya ugaidi, na kwamba pingamizi lililowasilishwa na upande wa utetezi halina mashiko na hakubaliani nalo.