Pindi Chana: Royal Tour ni lango la fursa za Utalii

0
268

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Pindi Chana, ametoa wito kwa Watanzania kuchangamkia fursa mbalimbali zitakazotokana na matokeo chanya ya Filamu ya Royal Tour inayo tarajiwa kuzinduliwa Jijini Arusha.

Dkt. Chana ameyasema hayo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), alipo wasili tayari kuhudhuria uzinduzi wa Filamu hiyo muhimu kwa sekta ya Utalii nchini.

“Royal Tour Arusha inakwenda kufungua zaidi fursa za Utalii nchini, Rais wetu Mpendwa Samia Suluhu Hassan ametufungulia fursa hii, sote tukae katika mkao wa kunufaika nayo”Amesisitiza Dkt. Chana

Filamu ya Royal Tour inatarajiwa kuzinduliwa hapa nchini jijini Arusha hapo kesho April 28,2022.