Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amesema ujenzi wa daraja linalounganisha sehemu ya Coco Beach na Agha Khan litachochea kasi ya uchumi kwa kuwa malighafi zake nyingi zitakuwa zinazalishwa na viwanda vya hapa nchini.
Makonda ameyasema hayo Jijini Dar es salaam wakati alipotembelea ujenzi wa daraja hilo ambalo linatarajiwa kukamilika mwishoni Oktoba mwaka 2021, daraja hili linatarajiwa kupunguza msongamano.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amefika kujionea maandalizi ta ujenzi wa daraja litakaloonganisha sehemu ya Coco Beach na Agha Khan na kubainisha kuwa malighafi zake nyingi zitakuwa zinatoka hapa nchini na kuwa chachu ya ukuaji kiuchumi hususani wa viwanda.
Vilevile Makonda amewashauri wa kazi wa Dar es salaam kujitathmini upya kuhusu maendeleo yanayoletwa na Rais Dkt. John Magufuli ambaye uchaguzi uliopita chama chake hakikupata wawakilishi wengi katika mkoa huo.
Naye Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ujenzi wa Barabara nchini – TANROADS Mhandisi Patrick Mfugale amesema ujenzi wa daraja hilo utagharimu zaidi ya dola za kimarekani milioni 100.
Baadhi ya wafanyakazi katika mradi huo wamesema fursa za ajira zimewafanya kuweza kujikimu kimaisha na hivyo kuwataka wenzao kuwa waaminifu katika utendaji wao wakazi.