Papa Francis ateua Mapadri wawili wa Tanzania kuwa Maaskofu

0
168

Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis amewateua Padri Henry Mchamungu na Padri Stephano Musomba kuwa maaskofu wasaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padri Charles Kitima inaeleza kuwa kabla ya uteuzi huo, Padri Mchamungu alikuwa mwalimu na mlezi wa Seminari ya Segerea jijini Dar es Salaam huku Padri Musomba, akihudumu kama Paroko wa Parokia ya Mavurunza jijini Dar es Salaam na Katibu wa Shirika la Waagustiniani Kanda ya Tanzania.