PAC: Tumeona thamani ya fedha miradi ya maji DAWASA

0
322

Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imeridhishwa na thamani ya fedha katika utekelezaji wa miradi ya majisafi katika mkoa wa Dar es salaam na mkoa wa Pwani

Kamati imeeleza hayo wakati ikikagua mradi wa maji Makongo hadi Bagamoyo uliogharimu kiasi shilingi bilioni 65 na kuonesha kuridhishwa na utekelezaji wa wake.

Kaimu Mwenyekiti wa PAC, Japhet Hasunga amesema “sisi kama kamati ya Bunge tumefanya ziara hii ili kuona na kutathmini thamani ya fedha zilizotolewa na Serikali katika mradi mbalimbali.”

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi DAWASA, Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange ameieleza kamati kuwa mojawapo ya siri yakufanikiwa katika utekelezaji wa miradi ya maji ni kutokana na uongozi mzuri uliopo na weledi mkubwa baina ya menejimenti na watumishi.

Mradi wa maji Makongo hadi Bagamoyo unatekelezwa kupitia fedha za wadau wa maendeleo na kusimamiwa na DAWASA kwa gharama ya shilingi bilioni 64.

Mradi utakapokamilika utahudumiwa wakazi zaidi ya 450,000 wa maeneo ya Changanyikeni, Vikawe, Goba, Bunju, Madale, Wazo, Ocean Bay, Salasala na sehemu ya mji wa Bagamoyo.