Othman kuendeleza misingi ya maridhiano

0
147

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, –  Othman Masoud Othman Sharif  amesema atatumia uzoefu alionao kumsaidia Rais wa Zanzibar Dkt Hussein Mwinyi kujenga na kuendeleza misingi ya maridhiano ya Umoja wa Kitaifa kwa maslahi ya Wazanzibar.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Zanzibar, – Othman amesema chini ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa atasaidia kuimarisha misingi ya sera katika nyanja mbalimbali ikiwemo kutengeneza sera bora ili kuleta maendeleo ya kiuchumi pamoja na kusimamia ustawi wa Wananchi.

Pia ameahidi kutumia uzoefu alionao Kimataifa katika kusimamia rasilimali za Taifa, uwekezaji pamoja na uwajibikaji katika taasisi za umma.

Othman Masoud Othman Sharif kutoka chama cha ACT Wazalendo ameapishwa mapema hii leo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Mwinyi kushika wadhifa huo kufuatia kifo cha Maalim Seif Sharif Hamad.