Omari Nundu afariki Dunia

0
153

Mbunge Mstaafu wa Tanga Mjini na Waziri wa zamani wa Uchukuzi,-Omary Nundu amefariki Dunia jijini Dar es salaam.

Taarifa zilizothibitishwa na Hospitali ya Taifa Muhimbili zimeeleza kuwa, Nundu alifikishwa hospitalini hapo kwa gari binafsi la kubeba wagonjwa akiwa tayari amekwishafariki Dunia.

Hivi karibuni, Rais John Magufuli alimteua Omary Nundu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Simu za Mkononi ya Airtel Tanzania,
kufuatia makubaliano yaliyofikiwa kati ya Serikali na kampuni ya Bharti Airtel International juu ya uendeshaji wa Airtel Tanzania.