Ole Nasha atema cheche Tanga

0
248

Naibu waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha amemuagiza Mkurugenzi wa jiji la Tanga, – Daudi Mayeji kumchukulia hatua Mhandisi wa jiji hilo Priscus Massawe kwa kosa la kubadilisha mchoro wa ujenzi katika shule ya sekondari ya Wavulana Galanos.

Naibu Waziri Ole Nasha ametoa agizo hilo baada ya kufanya ziara shuleni hapo na kukuta ujenzi ukiendelea Kwa kutumia tofali badala ya chuma kama ilivyotakiwa katika mchoro.