Ofisi za CCM Tabora zapata ugeni wa Rais

0
202

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Rais Samia Suluhu Hassan ametembelea ofisi za chama hicho mkoani Tabora na kufanya mazungumzo na kamati ya siasa ya mkoa huo.

Pamoja na mambo mengine amepokea taarifa ya mwenendo wa uchaguzi ndani ya CCM unaoendelea, na kujadiliana masuala mbalimbali yenye ustawi na chama hicho na wananchi wa mkoa wa Tabora.

Awali Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tabora, Hassan Wakasuvi alimueleza Mwenyekiti huyo wa CCM Taifa kuwa wananchi wa mkoa huo wanaridhishwa na utendaji wa serikali ya awamu ya sita katika kuimarisha utoaji huduma, ujenzi wa miundombinu na ukuzaji wa uchumi kwa wananchi.

“Nimekuwa mwanachama wa chama hiki na kiongozi kwa miaka 25 lakini tukio la Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutembelea ofisi za chama chetu na kuzungumza na viongozi wake hili ni tukio la kwanza kwa mkoa wa Tabora, haya ni mahusiano mazuri baina ya chama na serikali.” amesema Wakasuvi

Rais Samia Suluhu Hassan yupo mkoani Tabora kwa ziara ya kikazi ya siku tatu.