Benki ya NMB imejipanga kuboresha huduma zake kwa kutafuta mbinu mbadala ya kuyafikia makundi yote kwenye jamii, ili yaweze kunufaika na mikopo inayotolewa na benki hiyo.
Mkuu wa kitengo cha Majanga na Mikopo wa NMB, Oscar Nyirenda ameyasema hayo mkoani Mtwara, wakati wa warsha iliyowakutanisha Wafanyabiashara kutoka mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma, lengo likiwa ni kufahamu changamoto mbalimbali zinazowakabili na namna ya kuzitatua.
Nyirenda amesema, hatua hiyo ya kuwakutanisha Wafanyabiashara hao pamoja inasaidia kufahamu matatizo mengi yanayowakabili ambayo NMB itaangalia ifanye kitu gani ili kuyamaliza.
Kwa upande wao baadhi ya Wafanyabiashara waliohudhuria warsha hiyo wameiomba benki ya NMB kuwapa mrejesho mara baada ya kuwasilisha changamoto zao.