Nini Tanzania inafanya kuendana na malengo ya viongozi wa Afrika?

0
110

Tanzania ni miongoni mwa nchi zaidi ya 40 zinazoshiriki mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Rasilimali Watu unaoendelea katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa mkutako huo Rais Samia Suluhu Hassan ameainisha baadhi ya maeneo ambayo Tanzania imeanza kuyafanyia kazi kulingana na malengo ya Afrika 2050 ambqyo ni;

Kutenga fedha katika afua za lishe na Wanawake, kuanzisha vituo vya awali vya elimu ya uzazi, mapitio ya sera ya elimu na mitaala, uanzishwaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kunusuru kaya masikini, uanzishwaji wa elimu bila ada kuanzia elimu msingi hadi sekondari na uwekezaji katika elimu ya ufundi na ujasiriamali.

Pia kuwaruhusu Wasichana waliopata ujauzito kurejea shuleni kuendelea na masomo, programu ya kilimo kwa ajili ya vijana pamoja na ufugaji na uvuvi.