NIMR na Aga Khan kushirikiana katika tafiti

0
323

Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa magonjwa ya binadamu NIMR kwa kushirkiana na Hospitali ya Aga Khan iliyopo jijini Dar es Salaam zimesaini mkataba wa Makubaliano ya kufanya utafiti juu ya magonjwa mbalimbali ya binadamu ikiwa ni pamoja na kuwajengea wanafunzi wa udaktari uwezo wa kufanya tafiti zenye tija kwa jamii.

Akizungumza mara baada ya kuweka Saini ya Makubaliano hayo Mkurugenzi Mkuu wa NIMR Profesa Yunus Mgaya amesema taasisi hiyo itafanya kazi bega kwa bega na Hospitali hiyo ili kuleta matokeo chanya kwenye sekta ya afya nchini.

Profesa Yunusu amesema ushirikiano huo utasaidia kuwawezesha wanafunzi wanaosoma shahada ya Pili, tatu na PHD kutumia rasilimali za maabara kufanya tafiti zao kwa ufanisi nakuleta matokea chanya kwenye sekta ya afya.

Aidha Profesa Mgaya amebainisha kuwa utafiti huo utagusa magonjwa madogo na makubwa hususani magonjwa yasio ya mbukiza hasa magonjwa ya saratani, kisukari, magonjwa ya akili, moyo na magonjwa na Kiribatumbo

Kwa Upande wake Mwakilishi wa Hospitali ya Aga Khan Dkt.Harison Chuwa amesema kupitia ushirikiano huo na NIMR utatoa fursa nzuri ya kubadilishana mawazo yenye tija kwenye sekta ya afya kwa Ustawi wa wananchi.