NIMENONG’ONA NA JENISTA KILICHOTOKEA KWENYE FAMILIA ZETU

0
174

Rais Samia Suluhu Hassan amesema janga la matumizi ya dawa za kulevya limeathiri familia nyingi bila ya kujali hadhi ya familia hizo, akimaanisha familia zenye hali duni na zisizo na hali nzuri.

Akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Duniani yaliyofanyika kitaifa mkoani Arusha Rais Samia amesema ;

“Wakati tunaangalia mchezo wa Inocenta hapa nilikuwa nanong’ona na waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Waziri Jenista.. namwambia lilitokea kwenye familia yangu na yeye ananiambia kilichopo ndani ya familia yake. Sasa tukisema kila mtu asimame aseme kwenye familia kuna nini familia nyingi zimeathirika bila kujali hadhi ya familia hizo”

“Ukisoma maandiko mengine unaambiwa watoto wa kimaskini ndio wengi wanabugia huko, lakini hata watoto wa kitajiri…… Hata watoto ambao kwao ni kuzuri wanaingia kwenye janga hili, tofauti ni kwamba mtoto ambaye kwao kuzuri atanusuriwa harakaharaka atapelekwa huko na huko atanusuriwa haraka… mtoto wa kimaskini atapita azunguke barabarani kama wale tumewaona wanamuita Inno njoo…. Kwa hiyo tofauti ipo hapo.” Amesema Rais Samia