Nimekuwa na amani moyoni baada ya mahojiano : Membe

0
182

Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje katika Serikali ya awamu ya Nne na kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Bernard Membe amesema kuwa, kuhojiwa na Kamati ya Maadili ya chama chake ni faida kwake pamoja na Chama

Akizungumza nje ya Makao Makuu ya CCM jijini Dodoma Membe amesema kuwa, mahojiano na Wajumbe wa Kamati hiyo yamemfanya kuwa na amani.

Amesema wakati wa mahojiano hayo amepata nafasi nzuri ya kujadili masuala ya Kitaifa na Kimataifa pamoja na kufafanua mambo kadhaa ambayo CCM ilitaka kuyajua.

“Nimepata nafasi nzuri ya kutoa mawazo ya yale mambo nilioombwa kutoa mawazo, kwa hiyo sasa hivi mimi na mke wangu tunaenda kula chakula kizuri sana, lakini niwaambie safari hii ya kuja Dodoma ilikuwa na manufaa makubwa sana sana kwangu, kwa chama na kwa Taifa letu”, amesema Membe.