Ni matokeo ya mwanzo

0
226

Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi mwaka 2022 kwa upande wa Tanzania Bara, Spika Mstaafu, Anne Makinda amesema matokeo ya sensa yatakayozinduliwa leo ni ya mwanzo, na kwamba matokeo zaidi yataendelea kutolewa kadiri taarifa zinavyochakatwa.

Amesema kuwa Serikali imeandaa mwongozo wa matumizi ya taarifa za Sensa ili kuchochea ukuaji wa uchumi na kuboresha maisha ya Watanzania ambao ndio walengwa wakubwa.

Amewasihi viongozi kutumia takwimu ambazo zinatolewa na ofisi za takwimu, kwani zitawapa mwongozo wa mambo gani ya kutilia mkazo, na mambo gani ya kuyaacha.

Makinda ameyasema hayo jijini Dodoma katika hafla ya uzinduzi wa matokeo ya awali ya sensa ya watu na makazi, mwaka 2022.