Nguyen na wenzake kulipa fidia ya shilingi bilioni 42

0
196

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliyopo jijini Dar es salaam, imemhukumu Mkurugenzi wa Kampuni ya Viettel Tanzania, – Son Nguyen na wenzake watano ikiwemo kampuni hiyo, kulipa fidia ya shilingi bilioni 42 baada ya kupatikana na hatia ya kuisabishia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) hasara ya shilingi bilioni 75.

Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu wa mahaksma hiyo Thomas Simba, baada ya washtakiwa hao kufanya makubaliano na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) ya kukiri mashtaka yao.

Katika kesi ya msingi namba 28 ya mwaka 2020, Wakili Mwandamizi wa Serikali akisaidiwa na jopo la mawakili wa Serikali wamedai kuwa, kati ya Juni 8 mwaka 2017 na Machi 26 mwaka huu katika maeneo ya Mikocheni jijini Dar es salaam na maeneo mengine ya nchi, washitakiwa hao kwa pamoja walitumia masafa ya redio bila kuwa na kibali kutoka TCRA.

Katika shtaka lingine la ukwepaji kodi, washtakiwa hao wanadaiwa kukwepa kulipa kodi kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania kwa kutumia mitambo ya masafa ya kimataifa bila kuwa na kibali maalumu na kuisababishia mamlaka hiyo hasara ya shilingi bilioni sabini na tano.

Aidha mahakama hiyo imewapiga faini ya Shilingi milioni 24 ama kwenda jela mwaka mmoja washtakiwa watano, huku mshitakiwa wa sita ambayo ni kampuni ya Viettel ikiamriwa kulipa shilingi bilioni thelathini ndani ya kipindi cha mwaka mmoja kama fidia kwa madai kuwa mshtakiwa huyo amekuwa mkosaji wa mara kwa mara.

Washtakiwa hao wamelipa faini ya shilingi milioni ishirini na nne kila mmoja, pamoja na fidia ya shilingi Bilioni 12 ambayo imelipwa kwa DPP.

Washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Nguyen Bihn Min, Ha Minh Tuan, Vu Van Tiep, Nguyen Thanh Cong na Kampuni ya Viettel Tanania NGUYEN THANH CONG na kampuni ya VIETTEL Tanzania, ambao kwa pamoja wamehukumiwa kwa makosa manne kati ya lkumi.