Nguli wa muziki Ismail Michuzi afariki dunia

0
2339

Mwanamuziki mkongwe wa muziki wa dansi nchini, Ismail Issa Michuzi (61) amefariki dunia leo asubuhi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam, alikokuwa akitibiwa maradhi ya tumbo.

Ismail alikuwa mmoja wa waanzilishi na viongozi wa Bendi ya Dar International chini ya Marijani Rajabu na pia alihudumu kama katibu wa bendi toka mwanzo wake hadi mwisho.

Baada ya Dar International kudumaa, Ismail alijiunga na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na kuingizwa katika Bendi ya Mwenge Jazz kama mpuliza tarumbeta.

Alitumikia JWTZ hadi alipostaafu takribani miaka sita iliyopita na kuhamia Tukuyu, Mbeya ambako alifanya kazi kwa muda na Radio Chai FM.

Taarifa zinaeleza kuwa mipango ya mazishi inafanyika Tabata Mawenzi, Dar es Salaam na taarifa kamili za maziko zitatolewa baadaye.