Ng’ombe Ranchi ya Mabale kupelekwa Oman

0
117

Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) imetenga eneo lenye ukubwa wa hekta 11 katika ranchi ya Mabale mkoani Kagera kwa ajili ya kunenepesha ng’ombe watakaokidhi mahitaji ya soko la ng’ombe hai zaidi ya 4,000 kwa mwaka nchini Oman.

Mwenyekiti wa Bodi ya Ranchi za Taifa, Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema kitalu cha mabale kitakuwa ni kituo kuu cha kuhifadhi ng’ombe bora kabla ya kupelekwa katika soko nchini Oman.

Bodi ya Wakurugenzi NARCO pia imetembelea Ranchi ya Taifa ya Misenyi na kujionea ufugaji bora wa makundi makubwa ya ng’ombe wa Serikali unaotekelezwa na Kampuni ya Ranchi za Taifa – NARCO, na kuwezesha Taifa kupata mapato